1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania: Wafuasi wa chama cha upinzani CUF wataka kuandamana jijini Dar es Salaam

29 Septemba 2009

Chama Kikuu cha upinzani Tanzania CUF kimepanga kufanya maandamano kudai kuweko tume huru ya uchaguzi.

https://p.dw.com/p/Jta7
Profesa Ibrahim Lipumba azungumza na waandishi ya habari mjini Dar es SalaamPicha: DW

Katika mkutano na waandishi wa habari hii leo mjini Dar es Salaam, mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani katika Tanzania, CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alitangaza kwamba kesho wafuasi wa chama chake watafanya maandamano yatakayopitia katika barabara za Dar es salaam hadi ofisi ya msajili wa vyama vya kisiasa kudai kuweko tume huru ya uchaguzi nchini Tanzania.
Othman Miraji alizungumza na Profesa Lipumba kutaka ufafanuzi zaidi juu ya madhumuni ya maandamano hayo.