1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taratibu mpya za uwekezaji katika Bundesliga

27 Machi 2015

Ligi kuu ya kandanda Ujerumani Bundesliga inaendelea kumulikwa kifedha, hasa ikilinganishwa na ligi nyengine.

https://p.dw.com/p/1Eya4
Fußball Bundesliga Logo
Picha: picture-alliance/dpa

Kanuni mpya iliyofichuliwa na wasimamizi wa ligi hiyo, inapunguza zaidi uwezekano wa kuwepo na uwekezaji mkubwa katika ligi hiyo.

Shirika linaloidhibiti Bundelsiga, DFL, limekubaliana kuhusu tatibu hizo mpya zinazofanya iwe vigumu kwa wawekezaji wanaotaka kununua vilabu. Hivi karibuni, wahusika wa tatu ambao ni makampuni ya kitaifa na watu binafsi wataruhusiwa tu kuhusika katika idadi ya juu ya vilabu vitatu pekee, na hawataruhusiwa kumiliki zaidi ya asilimia 10 ya hisa katika mojawapo ya vilabu hivyo.

DFL imesema taratibu hizo zimechukuliwa kwa ajili ya kile imesema ni „kulinda uadilifu na uaminifu wa ushindani wa michezo“.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu