1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tarehe ya uchaguzi bado Kitendawili

1 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/Cilg

ISLAMABAD

Tume ya uchaguzi nchini Pakistan kwa mara nyingine imeshindwa kufikia uamuzi juu ya ikiwa uchaguzi wa bunge uliopangiwa kufanyika tarehe 8 mwezi huu ukhairishwe au la.

Kutokana na hali hiyo tume imesema itatangaza uamuzi wake hapo kesho baada ya kufanya mashauriano na vyama vya kisiasa.

Tarehe ya kufanyika uchaguzi huo inaangaliwa kuwa suala muhimu katika kuleta demokrasia nchini Pakistan amabko kumekuwa na hali ya machafuko tangu kuuwawa kwa kiongozi muhimu wa upinzani waziri mkuu wa zamani Benazir Bhutto.

Hata hivyo vyama vya upinzani vinasema vinataka kuona uchaguzi huo ukifanyika tarehe iliyowekwa ingawa inaonekana uchaguzi huo utasogezwa mbele kwa wiki kadhaa.Zaidi ya watu 40 wameuwawa katika ghasia zilizozuka siku kadhaa baada ya kuwawa kwa Bhutto wiki iliyopita.