1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TARO ASO.

Abdu Said Mtullya24 Februari 2009

Waziri Mkuu wa Japan leo anatarajiwa kuwa kiongozi wa kwanza kutoka nje kukutana na rais Barack Obama katika Ikulu ya Marekani.

https://p.dw.com/p/Gzzl
Waziri Mkuu wa Japan Taro Aso.Picha: AP

WASHINGTON.

Waziri Mkuu wa Japan Taro Aso amewasili  Washington kuwa  kiongozi wa kwanza kutoka  nje  atakaekutana  na rais Barack Obama katika Ikulu ya Marekani.

Waziri mkuu Aso  anaefanya  ziara  ya siku moja  nchini Marekani  anatarajiwa kukutana  na rais Obama leo.

Viongozi hao  wanatazamiwa kujadili njia za  kukabiliana  na  mgogoro wa fedha ulioikumba dunia.

AFP.