1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN: Acheni kiburi,Ahmednejad ayaambia mataifa makubwa

1 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCDZ

Rais Ahmednejad wa Iran ameyataka mataifa makubwa yaombe radhi badala ya kufanya kiburi kuhusiana na mgogoro uliosababishwa na kukamatwa mabaharia 15 wa Uingereza .

Rais Ahmadnejad amesema hayo kujibu kauli ya rais George Bush juu ya mgogoro huo.

Rais Bush amelaani hatua ya Iran kuwakamata mabaharia hao na kuilezea hatua hiyo kuwa kitendo kisichosameheka.

Rais Bush amesema kuwa mabaharia hao wametekwa nyara, na kuwa Marekani inaiunga mkono thabiti serikali ya Uingereza katika mgogoro huo.