1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN: Iran imefanikiwa kurusha roketi angani

25 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOg

Iran imetangaza kuwa imerusha angani roketi yake ya kwanza.Stesheni ya televisheni ya taifa imesema,jaribio la Iran kurusha roketi ya angani imefanikiwa,lakini haikueleza ikiwa roketi hiyo inahusika na mradi wake wenyewe wa satalaiti uliotangazwa.Wakati huo huo,kiongozi wa kituo cha utafiti wa safari za angani cha Iran,Mohsen Bahrami amesisitiza kuwa roketi hiyo inabeba zana za utafiti zilizoundwa na wizara za sayansi na ulinzi.Miaka miwili iliyopita,Iran kwa kushirikiana na Urussi ilirusha angani satalaiti yake ya kwanza.