1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Teheran: Iran inasema wanamaji wa Uingereza waungama

25 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFS

Maafisa wa kijeshi wa Iran wamedai kwamba waingereza 15 kutoka manowari ya Uingereza waliokamatwa katika Ghuba la Uajemi, wamekiri kwamba waliingia katika eneo la maji la Iran kinyume cha sheria. Uingereza inasema wanamaji hao walikamatwa wakati wakiwa katika shughuli zao za kawaida za kikazi katika eneo la maji la Irak. Uingereza na Ujerumani ambayo ni mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Ulaya, zimetaoa wito wa kuachiwa huru wanamaji hao. Wanajeshi wa Iran waliwatia nguvuni wanamaji hao 15 wa Uingereza siku ya Ijumaa katika eneo la maji la Shaat al-Arab, lilioko katika mpaka wa kusini kati ya Irak na Iran.