1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN: Iran kuendelea na mpango wake wa kinyuklia

23 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzs

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad, kwa mara nyingine tena ametangaza kuwa nchi yake itaendelea na mpango wake wa kinyuklia licha ya vistiho vya vikwazo vya Umoja wa mataifa. Akizungumza kwenye televisheni ya serikali, rais Ahmadinejad amesema taifa zima linaomba kutumia nguvu za nyuklia.

Wakati huo huo, waziri mkuu wa Israeli, Ehud Olmert, ameitolea mwito jumuiya ya kimataifa kumtenga rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad na kwamba jumuiya ya kimataifa ingepaswa kuchukuwa hatua wakati rais wa Iran anatoa mwito wa kuliangamiza taifa la Israeli.

Matamshi hayo ya wsaziri mkuu wa Israeli Ehud, Olmert, yametolewa wakati Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimetayarisha mswada wa sheria wa vikwazo ambao utawasilishwa mbele ya Baraza la usalama la Umoja wa mataifa kufuatia msimamo wa Iran kukataa miito ya kusimamisha kurotubisha madini ya Uranium.