1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN: Wito wa Umoja wa Ulaya wakataliwa

31 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCDo

Iran imeukataa wito wa Umoja wa Ulaya wa kuitaka nchi hiyo moja kwa moja iwaachilie huru wanamaji wa Kingereza waliokamatwa juma moja lililopitwa. Waziri wa masuala ya nje wa Iran amesema,Umoja wa Ulaya usiingilie kati mgogoro huo.Mawaziri wa nje 27 wa Umoja wa Ulaya waliionya Iran kuwa hatua zinazostahilika zitachukuliwa ikiwa wanamaji hao hawatoachiliwa huru upesi.Kwa mujibu wa Teheran,wanamaji hao wa Kingereza waliingia katika eneo la bahari la Iran,lakini Uingereza inasema,wanamaji hao walikuwa katika eneo la Irak.Kwa upande mwingine,Marekani imepinga uwezekano wa kubadilishana wanamaji hao 15 wa Kingereza na wale maafisa 5 wa Kiirani waliozuiliwa na majeshi ya Kimarekani nchini Irak tangu mwezi wa Januari.