1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERANI

5 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuZ

Rais wa Iran Mahamoud Ahmednejad amelionya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwazo zaidi Iran akisema uamuzi huo ni sawa na kuuchezea mkia wa Simba.

Matamshi hayo ya Ahamednejad yamekuja mnamo wakati ambapo afisa mkuu wa masuala ya kiusalama wa Iran Ali Larijan akikutana na waziri wa nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeir mjini Berlin.

Mazungumzo hayo ni muendelezo wa mazungumzo ya wiki iliyopita kati ya Larijan na mkuu wa siasa za nje wa Umoja wa Ulaya Javier Solan, kuhusiana na mpango wa nuklia wa Iran.

Mpango huo wa nuklia wa Iran unatarajiwa kuwa moja ya agenda muhimu katika kikao cha kesho cha wakuu wa nchi zilizoendelea zaidi kiviwanda duniani G8 mjini Hailegendamm Ujerumani.