1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN : Ahmedinejad ataka mazungumzo na Bush

24 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7k

Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran hapo jana amependekeza kuwa na mazungumzo na Rais George W. Bush wa Marekani ikiwa ni pendekezo la kushangaza kutoka kwa kiongozi huyo wa msimamo mkali ambaye nchi yake inazozana na Marekani kutokana na mpango wake wa nuklea unaobishiwa na kujihusisha kwake nchini Iraq.

Wakati hayo yakiripotiwa na kituo cha taifa cha televisheni ya Kiarabu cha satalaiti cha Iran tovuti ya Al-Alam imemkariri Ahmedinejad akisema kwamba mwaka jana alitangaza kuwa yuko tayari kuwa na mjadala wa moja kwa moja kwenye televisheni juu ya masuala ya dunia na mheshimiwa Bw. Bush na kwamba hivi sasa anatangaza kuwa yuko tayari kuzungumza na Bush juu ya masuala ya nchi zao kadhalika masuala ya kanda na ya kimataifa.

Kiongozi huyo wa Iran hakufafanuwa ni juu ya masuala gani hasa anataka kuzungumza na Bush lakini amesema mazungumzo hayo yanapaswa kufanyika mbele ya vyombo vya habari.

Haikuweza kufahamika mara moja iwapo kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ambaye ana usemi wa mwisho juu ya masuala yote ya taifa anaunga mkono pendekezo hilo la Ahmedinejad.