1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Iran haimtaki mkaguzi wa nishati ya kinyuklia.

27 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXd

Iran imesema inataka mkaguzi mmoja mkuu wa miradi ya nishati ya nyuklia aachishwe waadhifa wake.

Serikali ya Iran imewahi siku zilizopita kumlenga Chris Charlier wa Ubelgiji inayemdai kuwa na chuki dhidi yake.

Iran imetowa madai hayo baada ya hatua yake ya kuwapiga marufuku wakaguzi thelathini na wanane wa mataifa manne ya magharibi juma lililopita.

Wakati huo huo afisa mmoja mkuu wa Marekani ameitahadharisha Iran dhidi ya kutekeleza mpango wake wa kustawisha tanuri lake ili kuzidisha urutubishaji wa madini ya uranium.