1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran: Iran inasema katu katu haitaachana na mradi wake wa kinyukliya

18 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQw

Iran leo ilisisitiza kwamba haina nia ya kuusitisha mradi wake wa kurutubisha madini yake ya Uranium, licha ya muda iliowekewa kufanya hivyo na Umoja wa Mataifa kukaribia kumalizika. Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni, Mohammad Husseini, alisema kusitishwa mpango huo ni jambo lisilokubalika, na kuna njia nyingine ya kuumaliza mzozo huo wa kinyukliya pamoja na Umoja wa Mataifa. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo limeiwekea Iran vikwazo kwa kushindwa kusitisha kurutubisha madini yake ya Uranium, limeiwekea Iran tarehe ya mwisho ya Februari 21 iusitisha mpango wake huo. Kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Khamenei, akitetea hatua ya nchi yake kuwa na nishati ya kinyukliya, alisema inahitajiwa kwa vile hifadhi ya mafuta na gesi ya ardhini ya nchi hiyo karibuni itamalizika.