1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Iran kukutana na Marekani kuhusu usalama wa Irak

20 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CP1x

Iran imekubali kufanya mazungumzo mapya na Marekani kuhusu hali ya usalama nchini Irak kufuatia ombi lililowasilishwa na Marekani.

Tangazo hilo limetolewa licha ya mivutano inayozidi juu ya mpango wa nyuklia wa Iran.

Marekani imesema Iran imesaidia kupunguza idadi ya silaha na wapiganaji wanaovuka mpaka na kuingia nchini Irak.

Nchi hizo mbili zilifanya awamu tatu za mazungumzo kuhusu usalama wa Irak mapema mwaka huu. Hata hiyo mazungumzo hayo hayakufaulu kwani Marekani na Iran zililaumiana kwa machafuko yanayoendelea nchini Irak.