1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Iran kupunguza ushirikano iwapo itawekewa vikwazo.

23 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgo

Mbunge mmoja mwandamizi wa Iran ameonya kuwa Iran itapunguza ushirikiano wake na shirika la umoja wa mataifa la kuchunguza matumizi ya teknolojia ya kinuklia iwapo baraza la usalama la umoja huo litapitisha azimio leo kuiwekea vikwazo.

Mkuu wa tume ya usalama nchini Iran ameliambia shirika la habari la Mer kuwa ushikiano wa Iran na shirika hilo la umoja wa mataifa la nishati ya Atomic utapunguzwa kwa kiwango cha vikwazo vitakavyowekwa. Baraza linatarajiwa kuamua leo iwapo uwekewe vikwazo mpango wa kinuklia wa Iran.