1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Iran kurutubisha uranium viwandani

10 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAv

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad amesema nchi yake iko tayari kuanza urutubishaji wa madini ya uranium kwa kiwango kikubwa katika viwanda.

Akizungumza kwenye sherehe ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu Iran ilipofaulu kurutubisha uranium katika kinu chake cha Natanz, rais Ahamadinejad amesisitiza kwamba Iran imetumia haki yake kisheria kwa mujibu wa sheria za kimataifa kuendeleza teknolojia ya nyuklia.

Serikali ya Tehran inadai mpango wake wa nyuklia ni wa matumizi ya amani na wala si vinginevyo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani nchini Marekani, Mark McComark, amesema uamuzi huo wa Iran kuanzisha urutubishaji wa uranium viwandani ni ukaidi zaidi dhidi ya jumuiya ya kimatiafa.

McComark amesema hotuba ya rais Ahamadinejad imedhihirisha kwamba vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran kuhusiana na mpango wake wa nyuklia ni halali.