1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Iran yaitolea onyo Ulaya.

5 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmF

Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad ametoa onyo kali kwa mataifa ya Ulaya kutoingilia mpango wa kinuklia wa nchi hiyo.

Katika hotuba mbele ya kundi la watu waliokuwa wakimshangilia katika mji wa Sari, Ahmedinejad ameyashutumu mataifa ya Ulaya kwa kujaribu kuzuwia haki ya Iran kwa kufanya juhudi za kuzuwia kazi ya kurutubisha madini ya Urani.

Ahmedinejad ameitahadharisha Ulaya dhidi ya kuchukua kile anachokiona kuwa ni hatua za uhasama, na kusema kuwa hatua yoyote ya kuingilia zaidi inaweza kuleta hatari katika uhusiano kati ya Iran na Ulaya.

Wakati huo huo , wiki kadha za mkwamo zimesitisha uamuzi wa umoja wa mataifa kuhusu vikwazo vitakavyowekewa Iran kwa kushindwa kusitisha kazi yake ya kurutubisha madini ya Urani.

Ujerumani, Ufaransa na Uingereza zimeendesha juhudi za kutafuta suluhisho kupitia majadiliano katika mkwamo huo.