1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Iran yashutumu vitisho vya mataifa ya magharibi.

15 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2c

Wizara ya mambo ya kigeni ya Iran imevieleza vitisho vya mataifa ya magharibi kutaka kuiwekea vikwazo kuhusiana na nia yake ya kupata teknolojia ya kinuklia kuwa ni vita vya kisaikolojia.

Tovuti ya televisheni ya taifa ya Iran imeripoti kuwa Mohammed Ali Hosseini amesema kuwa Iran haitishiki na vitisho hivyo na kurudia azma ya taifa lake kuendelea na mpango wake wa kinuklia.

Mawaziri 25 wa umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukutana siku ya Jumanne kujadili kulitaka baraza la usalama la umoja wa mataifa kuiwekea vikwazo, kwa mujibu wa waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier.

Hata hivyo , Steinmeier jana Jumamosi amesisitiza kuwa vivutio ambavyo Iran imepewa vyenye lengo la kuishawishi kusitisha shughuli za urutubishaji wa madini ya Urani bado vinaendelea.