1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Masuala kuhusu uwezo wa roketi ya Iran

25 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOc

Shaka za mwanzo zimechomoza,ikiwa roketi iliyorushwa na Iran ina uwezo wa kuingia angani, kama ilivyodaiwa hapo awali na stesheni ya televisheni ya nchi hiyo.Makamu mtendaji wa shirika la Iran la utafiti wa misafara ya angani, Ali Akbar ameliambia shirika la habari la FARS kuwa roketi hiyo inaweza kwenda juu umbali wa kilomita 150 kabla ya kuanguka ardhini kwa mwavuli.Inasemekana kuwa roketi hiyo imebeba zana za utafiti.