1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Mtalii wa Kijerumani aachiliwa huru

13 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJb

Mtalii wa kijerumani aliyekamatwa pamoja na mwanamume wa kifaransa baada ya boti lao kuingia eneo la Iran ameachiliwa kutoka jela moja ya mjini Tehran.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, amethibitisha kuachiliwa huru kwa mjerumani huyo.

Donald Klein, mwenye umri wa miaka 52, alihukumiwa kifungo cha miezi 18 jela mnamo Januari mwaka jana pamoja na mfaransa, Stephanie Lherbier, kwa makosa ya kupiga picha meli katika ghuba ya Persia.

Lherbier alisamehewa na kuachiliwa mwezi uliopita.