1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Rais wa Iran aionya Ulaya.

20 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0o

Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad ameyaonya mataifa ya ulaya kuwa yanachochea hisia za chuki katika mashariki ya kati kwa kuiunga mkono Israel na kusema yanaweza kudhurika iwapo hasira katika eneo hilo itapindukia.

Ahmedinejad ametabiri kuwa Israel haitanusurika na kwamba washirika wake watakumbana na hasira hiyo ya watu iwapo wataendelea kuliunga mkono taifa hilo la Kiyahudi.

Ahmedinejad amerudia kuwa hali ya baadaya ya vita vikuu vya pili vya dunia haipaswi kuwa na athari katika dunia ya leo, na kwamba Wapalestina hawapaswi kubeba mzigo wa kitu chochote kilichotokea wakati wa mauaji ya halaiki ya Wanazi ya Holocaust.