1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Ubishi kati ya Iran na Uingereza bado waendelea

2 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCDH

Ubishi kati ya Iran na Uingereza kuhusu kukamatwa wanamaji 15 wa Uingereza umeingia katika siku yake ya kumi huku kukiwa hakuna ishara zozote za kupatikana suluhisho la haraka.

Televisheni ya Iran imeonyesha picha mpya za wanamaji wawili kati ya 15 wa Uingereza na ambao wamekwamtwa na kuzuiliwa nchini Iran.

Katika picha hiyo mpya wanamaji hao wamekiri kwamba walikamatwa katika eneo la pwani ya Iran.

Kituo cha televisheni cha taifa nchini Iran cha Al-Alam kimewaonyehsa askari hao wawili wa Uingereza Luteni Felix Carmen na Kapteni Chris Air ambao wamesema kuwa hawajatendewa vitendo vyovyote vya kinyama tangu walipokamatwa siku kumi zilizopita.

Wakati huo huo juhudi za kuachiliwa askari hao zikiendelea takriban wanafunzi 200 wamefanya vurugu nje ya ubalozi wa Uingereza mjini Tehran kupinga hatua ya wanamaji hao wa Uingereza kuingia katika eneo la pwani ya Iran.