1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Wanamaji wa Uingereza wakiri walifanya makosa

2 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCDA

Televisheni ya Iran imeonyesha picha mpya za mabaharia wawili miongoni mwa wanamaji 15 wa Uingereza wanaozuiliwa mjini Tehran.

Katika picha hizo mabaharia hao wameonekana wakikiri kwamba walikamatwa baada ya kuingia eneo la bahari lililo himaya ya Iran.

Televisheni ya Al-Alam inayomilikiwa na serikali ilionyesha picha za wanaume hao wawili wakiwa wamevaa sare wakisimama mbele ya ramani kubwa ya ghuba la Uajemi.

Luteni Felix Carmen na kapteni Chris Air, waliongeza kusema kwamba wamekuwa wakishughulikiwa vizuri tangu walipokamatwa siku kumi zilizopita.

Sambamba na taarifa hizo, redio ya serikali ya Iran imetangaza leo kwamba mabaharia wote 15 wa Uingereza wamekiri walifanya makosa kwa kuingia katika himaya ya Iran.

Juhudi za kidiplomasia zinaendelea ili mabaharia wote waachiliwe huru.