1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Watu 18 wauwawa katika shambulio la bomu

14 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSK

Vyombo vya habari nchini Iran vimeripoti kwamba watu 18 wameuwawa katika shambulio la bomu dhidi ya basi kusini mashariki mwa nchi hiyo. Basi hilo lilikuwa limewabeba walinzi wa mapinduzi, lakini haikubainika wazi ikiwa waliouwawa walikuwa walinzi.

Kwa mujibu wa walioshuhudia shambulio hilo, wanamgambo waliweka motokaa iliyokuwa na bomu katika barabara ilikopitia basi hiyo na kuiripua wakati basi ilipokuwa ikipita.

Shambulio hilo limefanywa mjini Zahedan karibu na mpaka wa Pakistan na Afghanistan, eneo ambalo linakabiliwa na mapigano makali baina ya maofisa wa usalama na makundi yenye silaha yanayohusika katika biashara ya madawa ya kulevya.