1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN:Iran na Urusi zaafikiana ushirikiano zaidi

17 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7F5

Rais wa urusi Vladimir Putin amekamilisha ziara yake nchini Iran jana usiku .Ziara hiyo iliimarisha zaidi uhusiano kati ya mataifa hayo mawili aidha Urusi kujitenga na kauli kali za mataifa ya magharibi kuhusu mpango wa Iran wa nuklia unaozua utata.Rais Putin alihudhuria mkutano wa mataifa yanayopakana na Bahari ya Caspian na kufanya mazungumzo na viongozi wa ngazi za juu wa Iran ikiwa ni ziara ya kwanza kufanywa na kiongozi wa Kremlin tangu vita vya dunia vya pili kumalizika.

Ziara hiyo ilikuwa na ulinzi mkali kufuatia madai ya njama ya kutaka kumuua Rais Putin.Bwana Putin aliyaonya mataifa ya magharibi kutoshambulia Iran kwasababu ya mpango wake wa nuklia na kusisitiza kuwa kiwanda cha kwanza cha nukilia cha Iran kilichojengwa na Urusi kitakamilika kama ilivyopangwa na kuunga mkono haki ya taifa hilo kutengeza nishati ya nuklia.

Taarifa ya pamoja ya viongozi hao inasisitiza umuhimu wa ushirikiano zaidi kuhusu masuala mbalimbali ulimwenguni.

Kauli hiyo ni tofauti kabisa na ya mataifa ya magharibi inayoshinikiza Iran kusitisha mpango wake wa nuklia na Umlja wa Mataifa kuiwekea vikwazo zaidi.Iran kwa upande wake inashikilia kuwa inalenga kutengeza nishati wala sio silaha za nuklia.