1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN:Iran yazionya nchi za magharibi

23 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNQ

Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran amezionya nchi za magharibi dhidi ya kuishambulia nchi yake kutokana na mpango wake wa nyuklia.

Kiongozi huyo wa jamuhuri ya kiislamu ya Iran amesema endapo nchi hizo zinadhania kwamba nchi yake itaathirika kimaendeleo kutokana na vikwazo vya kiuchumi na vitisho basi nchi hizo zinajidanganya na zinafanya kosa kubwa.

Matamshi ya rais Ahmedinejad yamefuatia siku moja tu baada ya wanadiplomasia wa nchi tano wanachama wa baraza la usalama la umoja wa mataifa na Ujerumani kukutana mjini Washington kujadili vikwazo zaidi ili kuilazimisha Iran isimamishe mpango wake nyuklia.

Rais Mahmoud Ahmedinejad anaelekea leo mjini New York ambako anatarajiwa kutoa hotuba mbele ya baraza kuu la umoja wa mataifa.