1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN:Mpatanishi wa Iran katika mazungumzo ya Nuklia Ali Larijani ajiuzulu

20 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7EC

Mpatanishi mkuu wa Iran kwenye mazungumzo juu ya mzozo wa Nuklia wa nchi hiyo na nchi za magharibi Ali Larijani amejiuzulu katika wadhifa huo.

Msemaji wa serikali Gholam Hossein Elham amesema Ali Larijani ambaye ni katibu wa baraza kuu la usalama la Iran amejiuzulu lakini hakuna sababu zilizotolewa kutokana na uamuzi huo ingawa msemaji wa serikali amesema bwana Larijani anataka kujishughulisha na masuala mengine ya kisiasa.

Rais Mahmoud Ahmedinejad amekubali kujiuzulu kwa Larijani na naibu waziri wa mambo ya nje anayehusika na masuala ya Ulaya na Marekani Saeed Jalili ndiye atakayechukua mahala pake.

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali wa Iran mazungumzo kati ya mjumbe wa Iran na mkuu wa sera za nje za Umoja wa ulaya Javier Solana yaliyopangiwa kufanyika jumanne yataendelea kama ilivyopangwa huko mjini Roma Italia.