1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN.Rais wa Iran asema ng'o hatikisiki wala hababaiki

26 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOJ

Rais Mahmoud Ahmednejad wa Iran amesema kuwa nchi yake haitarudi nyuma katika mpango wa nyuklia na kuufananisha mpango huo wa nyuklia sawa na treni isiyokuwa na breki.

Awali waziri wa mdogo wa mambo ya nje wa Iran alinukuliwa na vyombo vya habari ya kwamba nchi hiyo iko tayari kukabiliana na nchi yoyote ya magharibi.

Matamshi hayo yanajitokeza huku nchi tano wanachama wa baraza la usalama la umoja wa mataifa NA Ujerumani, zikipanga kukutana leo hii kujadili juu ya vikwazo zaidi dhidi ya Iran.

Wakati huo huo nchi kadhaa za kiislamu ikwemo Saudi Arabia zimeonya juu kupamba moto kwa mzozo huo na kupendekeza suluhisho kwa njia za kidiplomasia.