1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN:Wanafunzi kushinikizwa kutoshirikiana na Marekani

26 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVi

Iran inaonya kuwa serikali itawabana wanafunzi wote wa chuo kikuu wanaoaminika kuwasiliana na uongozi wa serikali kwa madhumuni ya kuipindua.Hayo ni kwa mujibu wa Waziri wa Usalama na Ujasusi Gholam Hossein Mohseni Ejeie.

Hivi karibuni uongozi nchini Iran unazidi kushinikiza wanafunzi na wahadhiri wa vyuo vikuu dhidi ya kushirikiana na uongozi wa Marekani huku hali ikiwa ya wasiwasi kwasababu ya mpango wake wa nuklia.

Vyuo vikuu nchini Iran vimezongwa na harakati za kisiasa huku wanafunzi 16 wakikamatwa mwezi Julai katika maadhimisho ya maandamano ya mwaka 99 pale wanachama wa kamati za uangalizi wa kiislamu walipovamia mabweni ya wanafunzi.

Majeshi ya usalama yaliwakamata wanafunzi 8 mwezi Mei wa Chuo Kikuu cha Amir Kabir kwa madai ya kuchapisha vibonzo vinavyokejeli uislamu katika gazeti moja la wanafunzi.Wanafunzi 3 kati yao bado wanazuiliwa jela na wengine waliosalia kauchiwa huru.Onyo kali la Waziri wa Usalama na Ujasusi linatokea wakati uchunguzi unaendelea kuhusu raia wa Marekani walio na asili ya Iran kulaumiwa kuwasiliana na taasisi za Marekani kuunga mkono juhudi za marekani za kuangusha uongozi wa Iran ulio na misingi ya kiislamu.

Mwanazuoni wa Mashariki ya kati Haleh Esfandiari na mtaalam wa mipango ya mji Kian Tajbakhsh wote walizuiliwa mwezi Mei kwa madai ya kuwa tishio kwa uslama wa kitaifa.Bwana Esfandiari aliachiwa kwa dhamana wiki jana.

Kulingana na kiongozi huyo wa usalama wa kitaifa wanafunzi hao watatu wa chuo kikuu Cha Amir Kabir bado wako jela kwani mashtaka yanayowakabili ya kukashifu Uislamu ni nyeti.