1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Teknolojia mpya kudhibiti wizi wa kura Kenya

Saumu Ramadhani Yusuf4 Machi 2013

Kenya imeanzisha teknolojia mpya itakayohakikisha kuwa uchaguzi wa Jumatatu unaendeshwa kwa uwazi na kuthibithishia ulimwengu kuwa taifa hilo la kanda ya Afrika mashariki linaweza kujikwamua na kurejesha hadhi yake

https://p.dw.com/p/17pWn
Election observers from the European Union Election Observation Mission (EU EOM) check ballot materials in a warehouse on February 13, 2013 in the Kenyan capital Nairobi, where they observed and had a discussion with poll-officials from the Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC). The March 4 polls are the first since bloody post-election violence five years ago, when what began as political riots quickly turned into deadly ethnic violence which as a result has steeped massive pressure on authorities to conduct a transparent elective process and has seen the east African nation employ modern systems such as biometrics in registration and polling processes. Kenya's foreign minister accused European diplomats on February 11 of trying to influence upcoming presidential elections, where a key candidate faces trial for crimes against humanity. AFP PHOTO / Tony KARUMBA (Photo credit should read TONY KARUMBA/AFP/Getty Images)
Waangalizi wa EU nchini KenyaPicha: Tony Karumba/AFP/Getty Images

Hatua hiyo ni jitihada nyingine ya kudhibiti vurugu kama za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 uliokumbwa na mzozo na kusababisha machafuko na vifo.

Waangalizi wa uchaguzi mara kwa mara katika chaguzi zilizopita wamekuwa wakiripoti wapiga kura bandia,masanduku ya kupigia kura kuwekwa makaratasi kabla ya uchaguzi na ukiukaji wa taratibu za uchaguzi. Lakini uchaguzi uliopita wa mwaka 2007 ndio uliokuwa mbaya zaidi kwani kulishuhudiwa umwagikaji damu huku karibu watu 1200 wakipoteza maisha yao baada ya wafuasi wa wagombea wawili wakuu kukabiliana.

Matumaini ya amani Kenya

Kenya haiwezi kurejea tena katika hali kama hiyo ya machafuko ya 2007 iliyosababisha taifa hilo linalosifika sana katika kanda hiyo ya Afrika mashariki kwa udhabiti wake wa kiuchumi kukwama na kuathiri pakubwa nyanzo za biashara za mataifa jirani. Wafadhili wa kutoka mataifa ya magharibi wana wasiwasi kuhusu Kenya,mshirika wao mkuu katika kanda hiyo hasa kuhusiana na vita dhidi ya makundi ya kigaidi.

Kenyan voters nominate people for political positions including those of MPs, governors and senators. Foto: Alfred Kiti, Nairobi, Kenia vom 17.01.2013
Uchaguzi wa ndani ya vyamaPicha: DW

Kipindi hiki,punde kura zitakapohesabiwa,matokeo kutoka kila kituo cha kupigia kura yatawasilishwa kwa tume ya uchaguzi kupitia njia ya kielektroniki na kuonyeshwa wazi kwa umma.Mfumo huo mpya ni kama ule uliotumika nchini Ghana katika uchaguzi wake mkuu mwaka jana,unaolenga kuondelea mbali makosa na kuzuia shutuma za udanganyifu.

Nafasi ya karatasi ya kupiga kura ipo

Bado kutatumiwa makaratasi ya kupigia kura ila wapigaji kura watatambuliwa kielektroniki. Simu zitakazotumika na maafisa wa uchaguzi katika vituo vya kupigia kura hazitakubali kutuma matokeo ambapo kura za jumla zinashinda zile zilizo kwenye sajili za wapiga kura wa eneo hilo. Hili la idadiya wapiga kura kutoingiliana na waliosajiliwa na tume ya uchaguzi lilikiwa suala lililozua malalamiko katika chaguzi zilizopita.

A voter marks a ballot paper at one of the polling stations. Photo by Alfred Kiti Copyright: DW
Raia mpiga kura nchini KenyaPicha: DW

Wagombea wawili wakuu wa urais Raila Odinga na Uhuru Kenyatta ambao wamejiunga na wagombea wengine sita kutoa wito wa amani,walifanya mikutano yao ya mwisho ya kujipigia debe hapo jana Juamamosi mjini Nairobi kabla ya siku ya mwisho ya kampeini kukamilika.

Mikakati kabambe yawekwa

Mkurugenzi  wa habari na mawasiliano wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC Dismas Ong´ondi amesema wameweka mikakati kabambe wakati huu ili kuzuia yaliyotendeka wakati uliopita yasijirudie akiongeza kuwa watu huingiwa na taharuki iwapo matokeo yanachelewa kutangazwa akitaja hili kuwa mojawapao ya malalamishi yaliyochangia ghasia za mwaka 2007.

Kipindi hiki matokeo ya awali huenda yakatangazwa saa chache baada ya vituo kufungwa. Hata hivyo tume ya IEBC ina siku saba kuambatana na sheria kutangaza matokeo rasmi.

Wengi wa wapiga kura milioni 14 wana imani na mfumo huo mpya wa kutumia teknoljia licha ya kuwa wengine wanahofia huenda kukazuka tena ghasi baada ya uchaguzi. Vile vile wana imani na idara ya mahakama ambayo imefanya marekebisho makubwa na kuwa huru na haki na hivyo wataweza kukabiliana na mizozo itakayochipuka.

Mbali na kumchagua rais,wapigaji kura wa Kenya watawachagua magavana, maseneta,wabunge,wawaikilishi wa kaunti na wawakilishi wa wanawake.

Mwandishi: Caro Robi/ Reuters
Mhariri: Saumu Yusuf.