1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEL AVIV: Israel yafunga vituo vingine vya mpakani

29 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7BV

Israel imeonya kuwa itazuia kila aina ya huduma kwa kiasi ya Wapalestina milioni 1,5 wanaoishi Ukanda wa Gaza,ikiwa mashambulizi ya makombora na magruneti yataendelea kufanywa dhidi ya Israel.

Afisa wa Kiisraeli amesema,hatua iliyochukuliwa na Israel kupunguza usafirishaji wa mafuta ya petroli kwa kama asilimia 15,ni onyo kwa chama cha Kipalestina chenye siasa kali-Hamas.

Israel vile vile imefunga kituo cha mpakani cha Suffa,kinachotumiwa kuingia Ukanda wa Gaza. Kufungwa kwa kituo hicho,kutaathiri vibaya mno usafirishaji wa bidhaa,sehemu ya kusini.Sasa kituo pekee kilichobakia wazi ni kile cha Kerem Shalom,karibu na mpaka wa Misri.