1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tel Aviv. Israel yaitaka jumuiya ya kimataifa kuisusia serikali ya Palestina.

19 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHb

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea na ususiaji wa serikali ya Palestina licha ya kuundwa kwa baraza jipya la mawaziri.

Olmert amesema kuwa serikali hiyo mpya inakosa kufikia madai ya jumuiya ya kimataifa ya kukana matumizi ya nguvu na kutambua haki ya Israel kuwapo.

Lakini ameahidi kuwa na mawasiliano na rais Mahmoud Abbas mwenye msimamo wa kati.

Serikali mpya ya Palestina inaunganisha kundi la wapiganaji la Hamas na kundi la Fatah la Abbas.

Ujerumani , ambayo inashikilia kiti cha urais cha umoja wa Ulaya , imesema kuwa umoja wa Ulaya unahitaji kupima matendo ya serikali hiyo mpya kabla ya kuamua iwapo kama irejee kutoa misaada tena.

Ubalozi mdogo wa Marekani mjini Jerusalem umesema Marekani haitakuwa na mawasiliano na mawaziri wa Hamas lakini wataruhusu mawasiliano na mawaziri kutoka chama kingine katika msingi wa masuala yaliyopo.