1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tel Aviv: Israil yatoa pendekezo la amani na Syria.

9 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtX

Maafisa wa serikali ya Israil wamesema Waziri Mkuu, Ehud Olmert, ameiahidi Syria kwamba nchi yake iko tayari kuondoka kwenye milima ya Golan iwapo Syria itakubali kutia saini mkataba wa amani kamili.

Duru za kibalozi zinasema kiongozi wa Syria hajasema lolote kuhusu mapendekezo hayo.

Israil iko tayari kuirejeshea Syria milima ya Golan iwapo nchi hiyo itakatiza uhusiano wake na makundi ya wanamgambo wa Kipalestina.

Vyombo vya habari nchini Israil vimesema mapendekezo hayo yaliwasilishwa kwa Syria kupitia maafisa wa kibalozi wa Uturuki na Ujerumani.

Israil iliiteka milima ya Golan wakati wa vita vya siku sita vya mwaka elfu moja mia tisa na sitini na saba.