1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEL AVIV : Maelfu wamtaka Olmert ajiuzulu

4 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4y

Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert ameendelea kun’gan’gania madaraka licha ya wito wa kumtaka an’gatuke kutoka sehemu kubwa ya wabunge na maandamano ya takriban watu 70,000 mjini Tel Aviv hapo jana.

Hatua hiyo inakuja kufuatia repoti kali ya tume ya uchunguzi ya Israel juu ya namna alivyoshughulikia vita vya mwaka jana dhidi wanamgambo wa Hizbollah nchini Lebanon vita ambavyo Israel iliboronga.

Kiongozi wa upinzani bungeni Benjamin Netanyahu ametowa wito wa kufanyika kwa uchaguzi mpya.Hapo Jumataano waziri wa mambo ya nje wa Israel Tzipi Livni wa chama chake mwenyewe Olmert cha Kadima ametowa wito hadharani wa kumtaka waziri mkuu huyo wa Israel ajiuzulu.

Hata hivyo hapo jana hakukuwa na kura bungeni ya kutokuwa na imani na serikali.

Wachambuzi wa mambo wanasema kwamba wanachama wa Kadima wanahofu kuwa iwapo utafanyika uchaguzi chama hicho kitashindwa.