1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tel Aviv. Mwanasheria ataka rais Katsav ajiuzulu.

29 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCy1

Mwanasheria mkuu wa serikali ya Israel amependekeza kuwa Moshe Katsav ajiuzulu kutoka wadhifa wake wa urais kabla ya matokeo ya uchunguzi kuhusu madai ya ubakaji.

Radio ya Israel imesema kuwa mwanasheria huyo wa serikali ametoa tamko hilo ambalo halina uwezo wa kisheria kutokana na uchunguzi wa mahakama kuu.

Katsav yuko chini ya uchunguzi baada ya polisi kusema kuwa kuna ushahidi unaomhusisha na ubakaji na bugdha kwa wanawake kadha waajiriwa. Rais huyo amekana kuwa na kosa lolote.