1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tel Aviv. Peres kugombea urais.

31 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwT

Naibu waziri mkuu wa Israel Shimon Peres ametangaza nia yake ya kugombea kiti cha urais mwezi ujao.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 83 ametoa tamko hilo katika mkutano na wabunge kutoka chama chake cha Kadima cha mrengo wa kati.

Hii itakuwa mara yake ya pili kutaka kuwa kiongozi wa juu katika taifa hilo.

Mara ya kwanza aligombea kiti hicho miaka saba iliyopita, lakini alishindwa na Moshe Katsav. Rais wa sasa amekuwa katika likizo ya kutokuwapo kazini tangu mwezi Januari, lakini amekataa kujiuzulu kutokana na madai ya ubakaji na ushambuliaji.

Anapata kinga ya kutokushitakiwa wakati akiwa katika wadhifa huo, lakini waendesha mashtaka wamesema kuwa watamshitaki wakati muda wake utakapomalizika.