1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEL AVIV: Rais wa Israil, Moshe Katsav, ashinikizwa ajiuzulu.

25 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCY3

Waziri Mkuu wa Israil, Ehud Olmert, amemtaka Rais Moshe Katsav ajiuzulu kwa tuhuma zinazomkabili za ubakaji na bughudha ya kijinsia.

Ehud Olmert amesema kwa hali ilivyo, Rais Moshe Katsav hana budi ila ang´atuke.

Hata hivyo rais huyo amesema hataondoka mamlakani hadi pale kesi dhidi yake itakapowasilishwa rasmi mahakamani.

Rais Moshe Katsav aliwaambia wanahabari kwamba madai yaliyotolewa dhidi yake hayana ukweli wowote.

Mwanasheria Mkuu wa Israil amesema rais huyo atafunguliwa mashtaka kadha yanayotokana na madai ya wafanyi kazi wake wa kike wa zamani.