1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tel Aviv. Rice akutana na waziri Livni.

2 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBd2

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice yuko mjini Jerusalem kwa mazungumzo na waziri mkuu Ehud Olmert pamoja na maafisa wengine waandamízi.Hiki ni kituo chake cha tatu katika ziara ya Rice katika mashariki ya kati, ambayo kwa sehemu ina lengo la kuweka msingi wa mkutano wa eneo hilo wa amani utakaofanyika katika majira ya mapukutiko.

Rice amesema kuwa katika mamlaka ya Palestina ipo serikali ambayo inakubali misingi ya kimataifa, ambayo ni misingi ya amani. Na hii ni nafasi ambayo haipaswi kutupwa. Ni wazi kwamba kile kilichotokea katika eneo la Gaza ni kinyume na taasisi halali za watu wa Palestina. Hata hivyo ameahidi kuwa jumuiya ya kimataifa haitawatupa mkono watu wa Gaza na hatima yao kuwaachia chama cha Hamas.Kufuatia mkutano wake na Rice, waziri wa mambo ya kigeni wa Israel Tzipi Livni amesema kuwa hii itakuwa ni nafasi adimu ya kupatikana amani.Hapo awali , Rice alikutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Saudi Arabia , mwanamfalme Saud al-Faisal mjini Jeddah.Kufuatia mazungumzo hayo , mwanamfalme aliwaambia waandishi wa habari kuwa Saudi Arabia itakuwa tayari kuhudhuria mkutano huo. Saudi Arabia inaunga mkono pendekezo la mataifa ya umoja wa Kiarabu , ambalo linatoa kwa Israel mahusiano kamili ya kidiplomasia ikiwa itaondoka kutoka katika maeneo ya ardhi za Waarabu ambazo inazikalia tangu katika vita vya mwaka 1967.