1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEL AVIV:Israel yaanza kuwaachia wafungwa wa kipalestina

20 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgn

Israel imeanza kuwaachia wafungwa kiasi cha 256 wa kipalelstina ikiwa ni sehemu ya mpango wa kumpa nguvu Rais Mahamud Abbas anayeungwa mkono na Marekani, na kuzidi kuwatenga mahasimu wake wa Hamas.

Basi likiwa na kundi la kwanza la wafungwa hao 120 linaelekea katika mjini wa Ramallah huko ukingo wa Magharibi, wengi wao wakiwa ni wale wanaotoka katika kundi la Fatah linaloongozwa na Rais Abbas.

Miongoni mwa wafungwa hao waliyoachiwa ni pamoja na wanawake sita na Abdul Rahim Malouh ambaye ni kamanda mkuu msaidizi wa tawi la chama cha FATAH la PLO, ambalo lilimua waziri mmoja wa Israel mwaka 2001.

Israel inawashikilia zaidi ya wapalestina elfu 11, na wengi wanasema kuwa idadi hiyo ya wafungwa waliyoachiwa hailingani na ile ya waliyo gerezani.

Wakati huo huo kundi la pande nne linalosaka amani katika mashariki ya kati limeunga mkono wito wa Rais George Bush wa Marekani kutaka kufanyika mkutano wa kimataifa kuzungumzia jinsi ya kufufua mazumgumzo ya amani kati ya Israel na Palestina.