1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TELAVIV:Wapalestina kusaidiwa

21 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpv

Waziri wa ulinzi wa Israel Ehud Barak ameliagiza jeshi la nchi yake liwaruhusu wapalestina wanaohitaji huduma za afya wapatiwe huduma hizo kwenye hospitali za Israel.

Waziri Barak ametoa agizo hilo kuhusiana na wapalestina 200 waliokwama kwenye mpaka wa Erez kwa zaidi ya wiki nzima wakijaribu kukimbia kutoka Ukanda wa Gaza.Baadhi yao ni wagonjwa na majeruhi.