1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tergat kugombea urais wa Kamati ya Olimpiki Kenya

Bruce Amani
31 Machi 2017

Aliyekuwa mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za marathon Paul Tergat anasema atawania kiti cha urais wa kamati ya Kenya ya Olimpiki – NOCK dhidi ya rais wa sasa Kipchoge Keino

https://p.dw.com/p/2aQAa
Brasilien Rio 2016 800 Meter Finale der Männer David Lekuta Rudisha
Picha: Reuters//D. Ebenbichler

Kamati ya Olimpiki ya Kenya imekumbwa na matatizo tangu michezo ya Olimpiki iliyoandaliwa mjini Rio de Janeiro, Brazil.

Paul Tergat siegt beim Berlin-Marathon 2003
Mwanariadha wa zamani Paul TergatPicha: AP

Tergat alishinda mataji matano mfululizo ya dunia katika mbio za nyika kutoka mwaka wa 1995 hadi 2000 na medali mbili za fedha za Olimpiki katika mbio za mita 10,000. Anahudumu kwenye kamati kuu ya olimpiki Kenya.

NOCK itafanya uchaguzi mnamo Mei 5 baada ya kuidhinisha mabadiliko kwenye katiba yake wiki hii kufuatia ombi la Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki.

Uongozi wa Keino uko chini ya uchunguzi baada ya maafisa wakuu wa NOCK kukamatwa kufuatia sakata la Olimpiki mjini Rio na kushitakiwa kwa wizi wa vifaa vya michezo na fedha.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman