1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tetemeko la ardhi lakumba mkoa mmoja wa Indonesia

7 Januari 2008
https://p.dw.com/p/ClYr

JAKARTA:

Tetemeko la ardhi ambalo limetokea katika eneo la mashariki ya Indonesia, limewajeruhi watu wanane na kusababisha mioto katika baadhi ya nyumba za mahali hapo.

Kitovu chake kimerikodiwa kuwa kilomita nane kaskazini mwa mji wa mwambao wa Manokwari katika mkoa wa Papua magharibi. Indonesia imekaa katika kile kinachoweza kuelezwa kama-duara ya moto ya Pasifiki,eneo ambalo ni hai mno kwa mitetemeko ya ardhi ya kila mara.