1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

THE HAGUE: Charles Taylor kufikishwa mahakamani leo

4 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBv5

Aliyekuwa rais wa Liberia Charles Taylor leo anatarajiwa kufikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa mjini The Hague Uholanzi.

Taylor anatuhumiwa kuwaunga mkono waasi nchini Sierra Leone waliotekeleza machafuko ya miaka 11 yaliyosababisha vifo vya maelefu ya watu.

Kesi hiyo inaendeshwa na mahakama maalum ya umoja wa mataifa ambayo ilihamishwa kutoka taifa hilo la Afrika ya Magharibi kwa sababu za kiusalama.

Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa Afrika kukabiliwa na mshtaka ya aina hii mbele ya mahakama.