1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

THE HAGUE:Taylor afika mahakamani kwa mara ya kwanza

3 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmH

Kiongozi wa zamani wa Liberia Charles Taylor, hii leo kwa mara ya kwanza amefika mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili ya uhalifu wa kivita, katika mahakama ya mjini the Hague Uholanzi.

Taylor ambaye aligoma kufika mahakamani toka kesi ilipotajwa mwezi mmoja uliyopita, kutokana na matatizo ya mawakili wake, aliwasili mahakamani hapo kabla ya majaji kuelezea sababu za kuahirishwa kwa kesi hiyo hadi tarehe 20 mwezi ijayo.

Majaji hao walikubaliana na upande wa utetezi pamoja na mwendesha mashtaka kuwa kesi hiyo isubiri jopo zima la upande wa utetezi likamilike.

Charles Taylor anatuhumiwa kukifadhili kikundi katili cha RUF kilichoendesha mauaji ya kikatili ikiwemo kuwakata viungo watu nchini Sierra Leone.Amekanusha mashtaka yote dhidi yake.