1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

THE HAGUE:Wabosnia wasikitishwa na uamuzi wa mahakama juu ya mauaji ya Srebrenica

27 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCO8

Baada ya mahakama ya kimataifa ya mjini The Hague hapo jana kupitisha uamuzi wa kuiondolewa lawama Serbia kwamba haijahusika moja kwa moja na mauaji ya halaiki ya waislamu wa Bosnia Herzegovina,huko Srebrenica,Viongozi wa kiislamu huko Bosnia wameelezea masikitiko yao juu ya uamuzi huo.

Mahakama ya The Hague imesema kwamba mauaji ya watu elfu 8 mwaka 1995 yalikuwa mauaji ya halaiki lakini serikali ya Belgrade haikuhusika moja kwa moja.

Mahakama hiyo badala yake imefahamisha kuwa Serbia ilivunja sheria ya kimataifa kwa kushindwa kuzuia mauaji hayo.

Kwa upande wake rais wa Serbia Boris Tadic amekubaliana na uamuzi wa mahakama hiyo na amelitaka bunge la nchi yake kulaani mauaji hayo ya halaiki ya Srebrenica.