1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

THE HAGUE:Watuhumiwa wa uhalifu wa kivita jimboni Darfur kutajwa leo

27 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOB

Mshtaki mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu anatarajiwa kuwataja watuhumiwa wa kwanza wa uhalifu wa kivita katika jimbo la magharibi mwa Sudan la Darfur.

Luis Moreno-Ocampo anatarajiwa kuwasilisha hii leo majina ya watuhumiwa hao pamoja na ushahidi dhidi yao kwa majaji wanaoshughulikia suala hilo kabla ya kufunguliwa mashataka.

Awali Ocampo alisema wachunguzi wake wamepata ushahidi juu ya ubakaji ,utesaji ,mauaji na unyanyasaji katika jimbo la Darfur.

Zaidi ya watu laki mbili wanasemekana waliuwawa katika mzozo wa Darfur na wengine milioni mbili na nusu walilazimika kuyahama makaazi yao tangu mwaka 2003 wakati waasi walipokuwa wakipambana na serikali ya mjini Khartoum.

Mwaka 2005 mwezi Marchi baraza la usalama la Umoja wa mataifa liliitaka mahakama ya kitamaifa ya uhalifu wa kivita kuchunguza mzozo huo.