1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tiger Woods arejea kileleni mwa Gofu

MjahidA26 Machi 2013

Mchezaji nyota wa Gofu wa Marekani Tiger Woods amewika tena baada ya kunyakuwa ubingwa katika mchezo huo hapo jana, hii ikiwa ni mara ya kwanza tangu nyota yake ilipoanza kuburuza mkia.

https://p.dw.com/p/184N4
Tiger Woods
Tiger WoodsPicha: Reuters

Ushindi wa Woods mwenye umri wa miaka 37 umempa nafasi ya kunyakuwa tena taji lake na kushika nafasi ya kwanza katika mchezo huo, taji lilokuwa likishikiliwa na mpinzani wake Rory McIlroy.

"Nimecheza vizuri, na ushindi huu unatokana na kutia bidii zaidi katika kazi yangu na kuwa na subira" alisema Woods. Ushindi wa jana Jumatatu umempatia nyota huyo wa gofu kitita cha euro milioni 1.08 million.

Baada ya Woods kukabiliwa na kashfa ya kimapenzi iliyozua sintofahamu kati yake na mkewe miaka mitatu iliyopita na hata majeraha ya mguu aliopata yalimfanya kuvuta mkia katika mchezo huo wa gofu ambao tangu alipoanza kuucheza mwaka wa 1997 amewaki kupata ushindi kwa mara 77.

Tiger Woods akicheza mchezo wa Gofu
Tiger Woods akicheza mchezo wa GofuPicha: AP

Novemba 11 mchezaji huyo alishuka katika kiwango cha chini kabisa na kuwa nafasi ya 58 duniani. Masaibu yake yalianza mwaka wa 2009 baada ya gazeti moja la udaku nchini Marekani kuandika kuhusu mahusiano yake na meneja wa klabu moja nchini humo. Siku mbili baadae kufuatia maswali mengi kuhusu ndoa yake, Wood alipata majeraha kutokana na kupata ajali karibu na nyumbani kwake.

Disemba mwaka huo Tiger Woods alitoa taarifa akikubali kuwa alikuwa na mahusiano nje ya ndoa yake na kutangaza kuwa anapumzika kutoka kwa mchezo huo wa Gofu. Baadaye alirudi uwanjani mwaka wa 2010, lakini ndoa kati yake na mwanamitindo wa zamani Elin Nordegren, ilikuwa imeshavunjika.

Wiki iliopita Woods alitangaza kuwa na mahusiano mapya na Lindsey Vonn Mmarekani ambaye ni mchezaji wa mchezo wa kuteleza kwenye barafu.

Mwandishi Amina Abubakar/AFP

Mhariri Mohammed Abdul-Rahman