1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu zaanza matayarisho Uefa Euro 2012

4 Juni 2012

Vikosi vya mataifa yanayoshiriki katika fainali za kombe la mataifa ya Ulaya vimo mbioni katika viwanja mbali mbali kujaribu vikosi vyao kwa ajili ya fainali za kombe la mataifa ya Ulaya.

https://p.dw.com/p/153LG
epa03204574 (FILE) General view of the Arena Lviv, Lviv, Ukraine, 12 April 2012. The stadium will host three preliminary round games of the UEFA EURO 2012. EPA/MARKIIAN LYSEIKO *** Local Caption *** 00000403179956 +++(c) dpa - Bildfunk+++
EM-Stadien 2012 Ukraine Stadion Arena LwiwPicha: picture-alliance/dpa

Ni wakati wa mwishoni mwa juma ambao utakuwa na heka heka nyingi za kandanda, kwa michezo ya kirafiki , ambayo itakuwa ni nafasi ya mwisho kwa wachezaji wengi walioteuliwa katika vikosi vya awali vya timu zinazoshiriki katika fainali za kombe la mataifa ya Ulaya , Euro 2012, kuonyesha ujuzi wao ili wajumuishwe katika vikosi hivyo, kabla ya muda wa mwisho uliowekwa na shirikisho la kandanda barani Ulaya UEFA kuwasilisha vikosi kamili vya timu hizo Jumanne ijayo.

Mabingwa watetezi Uhispania itakuwa katika mji wa St. Gallen nchini Uswisi ikiwa na vijana kadha wapya ambao wanatarajiwa kumuonyesha kocha Vicente Del Bosque umahiri wao ili waweze kujumuishwa katika kikosi hicho.

Wakati wachezaji kadha wa kikosi cha kwanza wakiwa katika timu za Barcelona na Athletic Bilbao ambao hawajajiunga na kikosi hicho , mlango uko wazi kwa wachezaji kama Juanfran na Adrian Lopez wa Atletico Madrid , Isco kutoka Malaga na mshambuliaji wa Sevilla Alvaro Negredo kujaribu bahati yao.

Danish National Soccer Team group photo, ahead of the frienly Match against Sweden at Parken Stadium in Copenhagen, Denmark, Friday, Nov. 11, 2011. Top from left, Thomas Sorensen (Stoke City), Nicklas Bendtner (Sunderland), Daniel Agger (Liverpool FC), Simon Poulsen (AZ Alkmaar), Andreas Bjelland (FC Nordsjaelland) and William Kvist (VfB Stuttgart). Bottom from left, Lars Jacbsen (FC Copenhagen), Dennis Rommedahl (Brondby IF), Christian Eriksen (AFC Ajax), Michael Krohn-Dehli (Brondby IF) and Niki Zimling (Club Brugge KV). The draw for the final tournament of the Euro 2012 is to be held on Friday, Dec. 2, 2011 in Kiev, Ukraine. (Foto:Lars Poulsen, POLFOTO/AP/dapd)
Timu ya taifa ya DänemarkPicha: dapd

Changamoto kubwa kwa Uhispania kutetea ubingwa wake hata hivyo itatoka Ujerumani, na kikosi cha Joachim Loew kinapambana jioni ya leo na Uswisi mjini Basel. Wachezaji wanne ni lazima waondolewe kutoka katika kikosi hicho cha Joachim Loew ambacho kwa sasa kina wachezaji 27, ambapo huenda mchezaji wa Borussia Dortmund Ilkay Gundogan na Julian Draxler wa Schalke 04 watafahamu iwapo watakuwamo katika kikosi hicho ama la. Meneja wa timu ya taifa ya Ujerumani Oliver Bierhoff hata hivyo amesema kuwa kipigo cha uchungu walichokipata Bayern Munich katika fainali ya Champions League hakiwezi kuiathiri timu ya taifa ya Ujerumani katika mashindano haya , lakini hali hiyo inatoa nafasi ya kuamka na kuwa macho kimichezo.

"Hii inatukumbusha kuchukua tahadhari kwa ajili ya mashindano ya kombe la Ulaya ,na nafikiri pia ni mawazo ya watu wengi. Ligi hii ya mapingwa imetuonyesha , kuwa sio suala la kujiamini kuwa huenda zile timu zinazopigiwa upatu kuwa zitanyakua kombe au timu bora ndio zinaweza kufanya vizuri. Tumeona ni kiasi gani hali imekuwa ngumu, tumeona kuwa ni mambo mangapi yanachangia kufanya vizuri na kwamba ni kiasi gani mchezo mzuri pia ni muhimu, lakini ni lazima kujaribu kuwa makini. Mtu anapswa kujaribu kupata matokeo. Hii inatosha kuona kuwa tunapaswa kuchukua tahadhari , wakati tukiingia katika fainali za kombe la mataifa ya Ulaya , kila mmoja anazungumzia tu Ujerumani au Hispania kuwa ndio timu bora zinazoweza kutoroka na taji hili la mataifa ya ulaya."

Fussball, Pressekonferenz der deutschen Nationalmannschaft vor dem Laenderspiel Ukraine - Deutschland, Donnerstag (10.11.11), NSC Stadion, Kiew, Ukraine: Der Manager der Fussball-Nationalmannschaft, Oliver Bierhoff, haelt ein Trikot mit der Aufschrift "Wir freuen uns auf 2012." in den Haenden. Die deutsche Fussball-Nationalmannschaft trifft in zwei Freundschaftsspielen am Freitag (11.11.11) in Kiew auf die Ukraine und am Dienstag (15.11.11) in Hamburg auf die Niederlande. (zu dapd-Text) Foto: Oliver Lang/dapd
Meneja wa timu ya taifa ya Ujerumani Oliver BierhoffPicha: dapd

Wakati huo huo Uholanzi , ambayo iko katika kundi B pamoja na Ujerumani inaikaribisha Bulgaria jioni ya leo mjini Amsterdam. Kocha Bert van Marwijk ameteua kikosi cha wachezaji 27. Kikosi hicho kinachojulikana kama Oranje, au rangi ya chungwa kinaanza juhudi zake za kutawazwa mabingwa wa euro 2012 dhidi ya Denmark Juni 9, na Denmark inakabiliana na Brazil katika mji wa Hamburg nchini Ujerumani leo Jumamosi. Kocha wa Denmark Morten Olsen hatakuwa akifanya majaribio ya wachezaji wake katika mchezo huu , amekwisha taja kikosi chake cha wachezaji 23 Alhamis wiki hii.

Bundestrainer Joachim Loew unterzeichnet am Dienstag (15.03.11) in Frankfurt am Main in der Zentrale des Deutschen Fussball-Bunds (DFB) seinen neuen Vertrag. Der DFB und Bundestrainer Joachim Loew werden ihre erfolgreiche Zusammenarbeit auch ueber die Europameisterschaft 2012 hinaus fortsetzen. Beide Seiten einigten sich auf eine vorzeitige Verlaengerung des im kommenden Jahr auslaufenden Vertrages bis zum 31. Juli 2014, wie der DFB am Dienstag mitteilte. Neben dem Bundestrainer unterschreiben auch sein Assistenztrainer Hansi Flick, Torwarttrainer Andreas Koepke sowie Teammanager Oliver Bierhoff neue Vertraege, die bis einschliesslich zur Weltmeisterschaft 2014 in Brasilien gelten. Foto: Ralph Orlowski/dapd
Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim LoewPicha: dapd

Brazil ambayo itakuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia mwaka 2014 wanatumia mchezo huu kama sehemu ya maandalizi kwa ajili ya mashindano ya Olympiki mjini London mwaka huu.

Uingereza inakwaana na Norway mjini Oslo katika mchezo ambao ni wa kwanza wa kocha Roy Hodgson.

Frank Lampard ni mmoja kati ya wachezaji kadha wa kikosi cha Hodgson kutoka moja kwa moja katika kushinda kombe la mabingwa wa Ulaya , Champions League akiwa na Chelsea na ana matumaini ya kuleta baraka hizo katika kikosi cha Uingereza. Lampard amesema iwapo tutaweza kuleta kiasi cha mchezo, hamasa , kutokata tamaa , na chochote kilichosababisha kushinda katika champions League katika kikosi cha Uingereza, nahisi hii inaweza kusaidia.

Ufaransa inawakaribisha Iceland kesho Jumapili katika mmoja kati ya michezo mitatu ya kirafiki ambapo kocha Laurent Blanc ameitayarisha kabla ya ufunguzi mchezo wa euro 2012 dhidi ya Uingereza Juni 11.

Tutafanya mabadiliko kadha katika kikosi chetu kitakachopambana na Iceland, Blanc amesema . Baada ya hapo tutaona kikosi chetu kitakachopambana na Uingereza kitakuwa vipi.

Kwingineko Jamhuri ya Ireland inakwaana na Bosnia- Herzegovina, wakati Urusi inamiadi na Uruguay. Ureno inakwaana na Macedonia, wakati wenyeji wenza wa euro 2012 Poland inakabiliana na Slovakai, na Jamhuri ya Czech inaumana na Israel na Uguriki inatiana kifuani na Slovenia. Ukraine inakabiliana na Estonia siku ya jumatatu.

Penalti ziondolewe?

Rais wa FIFA Sepp Blatter amemtaka mchezaji nyota wa zamani wa Ujerumani Franz Beckenbauer na jopo lake la wataalamu kujaribu kutafuta njia mbadala ya mikwaju ya penalti katika azma ya kuamua nani mshindi kwa timu zilizokwenda sare hata baada ya dakika 120 za mchezo.

Blatter alikuwa akizungumza na wajumbe katika mkutano mkuu wa FIFA siku ya Ijumaa wiki moja baada ya Chelsea kuishinda Bayern Munich kwa mikwaju ya penalti na kushinda kombe la mabingwa wa Ulaya, Champions League katika fainali mjini Munich.

Schlechte Zeiten für Sepp Blatter: Fünf Tage vor der Wahl des Vorsitzenden hat die Ethikkommission der Fifa eine Untersuchung gegen den Präsidenten angekündigt - auf Antrag seines Herausforderers Mohamed bin Hammam. FIFA ermittelt gegen Sepp Blatter.FOTOMONTAGE.
Rais wa FIFA Joseph Sepp BlatterPicha: picture alliance/Sven Simon

Kandanda ina weza kugeuka kuwa maafa wakati mchezo unaingia katika hatua ya penalti. Kandanda ni mchezo unaojumuisha kikosi kizima na iwapo utaamuliwa kwa kupambana mtu mmoja mmoja, inapoteza msingi wake, Blatter amesema. Huenda Beckenbauer na kundi lake la "Football 2014", anaweza kutupatia suluhisho, huenda sio leo lakini hapo baadaye.

Na wakati huo huo taifa jipya lililojipatia uhuru wake mwaka jana la Sudan ya kusini imekuwa mwanachama rasmi wa 209 wa shirikisho la kandanda duniani FIFA, baada ya kupigiwa kura kuingia katika shirikisho hilo na wajumbe wa FIFA katika mkutano wao wa mwaka. Sudan ya kusini ambayo ilitengana na Sudan na kuwa taifa huru Julai mwaka jana , imejiunga na shirikisho la kandanda barani Afrika CAF Februari mwaka huu na kuwa na nafasi ya kujiunga na FIFA baada ya FIFA kuondoa sheria yake ya kusubiri kwa miaka miwili kwa wanachama wapya.

Georgia na Azerbaijan zimerudia nia yao ya pamoja ya kuwania kuwa wenyeji wenza wa fainali za kombe la mataifa ya ulaya , euro 2020 wamesema maafisa mjini Baku na Tbilisi wiki hii.

Juhudi hizo za pamoja zilitangazwa March mwaka huu lakini Azerbaijan ilijitoa kwasababu ilikuwa pia inawania kuwa mwenyeji wa mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2020, na kuiacha Georgia kuwania uwenyeji huo peke yake. Lakini baada ya juhudi za Azerbaijan kushindwa katika olimpiki baada ya mji mkuu wa Baku kuondolewa wiki hii, nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta na gesi iliamua kurejea katika uwenyeji wa fainali za Euro 2020 pamoja na Georgia.

Riadha.

Mkuu wa kamati ya riadha nchini Kenya (NOC), Kipchoge Keino ameshutumu vikali wiki hii ripoti iliyotolewa katika vyombo vya habari nchini Ujerumani ikituhumu kuwa kuna baadhi ya wanariadha wa Kenya ambao wanatumia madawa ya kuongeza nguvu. Keino amepuuzia madai hayo yaliyotangazwa na kituo kimoja cha televisheni nchini Ujerumaji kuwa ni njama za kuwavuruga wanariadha wa Kenya katika maandalizi yao kwa ajili ya mashindano ya Olimpiki ya mjini London mwaka huu.

Ripoti hiyo ya kituo cha televisheni cha Ujerumani imewahusisha baada ya wakimbiaji wa Kenya na madaktari ambao wamefanya doping ya damu , hatua ambayo inatumika kuongeza idadi ya seli nyekundu katika damu ili kuimarisha uwezo wa mkimbiaji.

Mwenyekiti wa chama cha riadha nchini Kenya Isaiah Kiplagat amesema kuwa wameanzisha uchunguzi kuhusiana na madai hayo , ambayo amesema kuwa ni juhudi za wivu tu kutaka kudharau uwezo wa wanariadha wa nchi hiyo.

Mwandishi;: Sekione Kitojo /rtre/afpe

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman