1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu zaendelea na maandalizi ya AFCON

5 Januari 2015

Maandalizi katika kombe la mataifa ya Afrika yanaendelea, ambapo timu mbali mbali zinazoshiriki mashindano hayo ya timu 16 nchini Guinea ya Ikweta yatakayoanza tarehe 17 mwezi huu zinatangaza vikosi vyake

https://p.dw.com/p/1EFGR
Africa Cup of Nations 2014 - Senegal vs. Ägypten
Picha: Khaled Desouki/AFP/Getty Images

Algeria imethibitisha leo kuwa imemuita kikosini Ahmed Kashi kwa mara ya kwanza katika kikosi hicho na mlinzi Liassine Cadamuro kuchukua nafasi za Essaid Belkalem na Mehdi Abeid ambao ni majeruhi.

Kashi , mzaliwa wa Ufaransa kutoka Metz hajawahi kuitwa katika kikosi cha Algeria, lakini Cadamuro , ambaye anaichezea klabu ya Osasuna nchini Uhispania, alikuwamo katika kikosi cha Algeria kilichoshiriki katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil mwaka jana pamoja na fainali ya kombe la mataifa ya Afrika nchini Afrika kusini miaka miwili iliyopita.

Mchezaji soka bora wa mwaka katika bara la Afrika atajulikana siku ya Alhamis wiki hii , wakati atakapotangazwa katika sherehe kubwa iliyoandaliwa mjini Lagos nchini Nigeria. Baadhi ya wachezaji wanaowania tuzo hiyo ni pamoja na mchezaji wa kati wa Manchester City na timu ya taifa ya Cote D'Ivoire Yaya Toure ambaye ni mchezaji bora wa sasa, Pierre Emerick Aubamiyang wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Gabon na Sofiane Feghouli wa Valencia ya Uhispania na timu ya taifa ya Algeria.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre , afpe , dpae
Mhariri: Iddi Ssessanga