1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu zajiandaa kwa nusu fainali

24 Juni 2013

Ukizitupia jicho timu zilizofuzu katika nusu fainali ya kombe la mabara – Confederations Cup, utaona mvuto wa dimba la mwaka huu kuwa kama ni kionjo cha fainali za kombe la dunia nchini Brazil hapo mwakani.

https://p.dw.com/p/18vAg
FORTALEZA, BRAZIL - JUNE 23: Jordi Alba of Spain (18) beats the Nigeria defence to score their first goal during the FIFA Confederations Cup Brazil 2013 Group B match between Nigeria and Spain at Castelao on June 23, 2013 in Fortaleza, Brazil. (Photo by Clive Rose/Getty Images)
Confed Cup 2013 Spanien gegen NigeriaPicha: GettyImages

Mabingwa wa dunia Brazil wanaangushana na washindi wa kwanza wa kombe la dunia Uruguay wakati mabingwa watetezi Uhispania wakicheza na washindi mara nne wa kombe la dunia Italia.

Neymar ni moto wa kuotea mbali

Shujaa wa nyumbani Neymar amewapa mashabiki msisimko, jinsi tu anavyoendelea kufanya mfungaji wa mabao mengi kwa sasa Fernando Torres wa Uhispania, Diego Forlan wa Uruguay na Andrea Pirlo na Mario Balotelli wote wa Italia.

Neymar amedhihirisha umahiri wake katika dimba hili, na hata kwa kucheza densi ya akicheza Samba
Neymar amedhihirisha umahiri wake katika dimba hili, na hata kwa kucheza densi ya akicheza SambaPicha: Getty Images

Na kwa wale waliosafiri kwenda Brazil kuangalia tu uhondo huo ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya kung'oa nanga dimba la kombe la dunia nchini Brazil, kama vile kocha wa timu inayopigiwa upatu Ujerumani, Joachim Löw, wameridhishwa na kinyang'anyiro hicho.

Uhispania wanakutana na Italia katika marudio ya fainali ya kombe la UEFA Euro 2012, wakati wenyeji Brazil wakipambana na Uruguay. Mpangilio huo una maana kuwa patakuwa na fainali kati ya timu kutoka Ulaya na Amerika ya Kusini katika uwanja wa Maracana.

Ushindi wa Uhispania wa mabao matatu kwa sifuri dhidi ya Nigeria uliwapeleka kileleni mwa kundi B na jumla ya pointi tisa na kuwakatia tikiti ya kuchuwana na nambari mbili wa kundi A Italia mjini Fortaleza siku ya Alhamisi.

Tahiti walikula jumla ya magoli 24 nao wakafunga moja tu

Uruguay iliwamiminia Tahiti magoli manane bila jawabu na kumaliza nambari mbili nyuma ya Uhispania, na kuwaweka mabingwa hao wa Copa America mwaka wa 2011 katika nusu fainali na Brazil mjini Belo Horizonte siku ya Jumatano. Brazil waliongoza kundi A na pointi tisa baada ya kuwazidi nguvu Italia mabao manne kwa mawili mjini Salvador Jumamosi iliyopita na kuwapa tabasamu mashabiki wa nyumbani.

Uruguay waliwamiminia Tahiti magoli manane kwa sifuri katika mechi ya mwisho ya makundi
Uruguay waliwamiminia Tahiti magoli manane kwa sifuri katika mechi ya mwisho ya makundiPicha: Getty Images

Kiungo wa Italia Andrea Pirlo atakuwa katika hali nzuri kushiriki mchuano wa nusu fainali baada ya kuwa nje pamoja na Daniele de Rossi aliyetumikia adhabu ya kucheza mechi moja. Hata hivyo kocha wa Italia Cesare Prandelli atalazimika kufanya mabadiliko katika safu ya mashambulizi kwa sababu mshambuliaji, Mario Balotelli ana jeraha la paja. Balotelli mwenye umri wa miaka 22 na ambaye amefunga mabao mawili katika dimba hili alitarajiwa kuongoza mashambulizi ya Italia katika lango la Uhispania.

Wakati washindi wa nusu fainali wakielekea Rio kwa fainali ya Jumapili, timu zitakazoshindwa zitakabana koo mjini Salvador siku hiyo hiyo kuamua mshindi wa nafasi ya tatu. Kuna wale wanaotabiri fainali kuwa kati ya wenyeji Brazil na mabingwa wa ulimwengu Uhispania….jinsi anavyoeleza shabiki huyu

Mwandishi: Bruce Amani/reuters/DPA

Mhariri: Yusuf Saumu